CUF siku zote itaongoza juhudi za wananchi zenye kuelekezwa katika kuiletea nchi yetu ukombozi wa kiuchumi. CUF itatilia maanani umuhimu wa rasilmali za nchi yetu kuwanufaisha wananchi wenyewe. Katika kufikia lengo hilo CUF itakuwa na uangalifu mkubwa katika kuwashirikisha wageni wenye uwezo wa fedha na teknolojia.